Sera ya Faragha
Sera hii inaeleza taarifa Bilima inazokusanya, sababu za matumizi yake na haki zako kuhusu akaunti, biashara, nyaraka na eneo.
Imesasishwa: 25 Julai 20261. Taarifa tunazokusanya
Tunakusanya taarifa za akaunti, biashara, mawasiliano, nyaraka za uhakiki, bidhaa, oda, malipo, vifaa na location pale ruhusa inapotolewa.
2. Jinsi tunavyotumia taarifa
Taarifa hutumika kuthibitisha biashara, kutoa huduma, kulinda transactions, kulinganisha suppliers na buyers, kutekeleza oda, kutuma notifications na kuboresha uaminifu wa jukwaa.
3. Eneo na faragha
Eneo kamili la buyer halionyeshwi kwa supplier kabla ya uhusiano wa kibiashara kukubalika. Live driver location huonekana kwa wahusika walioidhinishwa wa delivery husika.
4. Nyaraka na usalama
Nyaraka binafsi hutolewa kupitia access iliyodhibitiwa. Bilima hutumia ruhusa za nafasi, audit logs, session controls na storage access controls kupunguza ufikiaji usioidhinishwa.
5. Kushirikisha taarifa
Taarifa hushirikishwa tu kwa wahusika wanaohitajika kutekeleza huduma, providers walioidhinishwa au pale sheria inapotaka. Hatutoi OTP, passwords au keys kwa biashara nyingine.
6. Uhifadhi na haki zako
Taarifa huhifadhiwa kwa muda unaohitajika kwa huduma, usalama, upatanisho na wajibu wa kisheria. Unaweza kuomba export, marekebisho au kufutwa kwa akaunti kupitia settings au support.
7. Mawasiliano
Kwa swali au ombi la faragha, tumia ukurasa wa Mawasiliano au support ndani ya akaunti yako ili ombi liweze kuthibitishwa na kufuatiliwa.