Bilima
Mwanzo
Bilima

Masharti ya Huduma

Masharti haya yanaeleza wajibu wa biashara na watumiaji wanaotumia Bilima kupata suppliers, kuagiza, kulipa na kusimamia usafirishaji.

Yamesasishwa: 25 Julai 2026

1. Akaunti na mamlaka

Mtumiaji lazima atoe taarifa sahihi, awe na mamlaka ya kuiwakilisha biashara na alinde njia zake za kuingia. Akaunti na ruhusa haziwezi kutumiwa na mtu asiyeidhinishwa.

2. Uhakiki wa biashara

Bilima inaweza kuomba nyaraka za biashara na utambulisho, kuhitaji taarifa zaidi, kukataa au kusimamisha akaunti pale taarifa haziwezi kuthibitishwa au kuna hatari ya matumizi mabaya.

3. Bei, bidhaa na oda

Supplier anawajibika kwa usahihi wa bei, stoo, maelezo ya bidhaa na masharti ya ofa. Mnunuzi anawajibika kukagua quotation na order kabla ya kuthibitisha.

4. Malipo na usafirishaji

Masharti ya malipo, pickup, delivery, deposits, refunds na gharama huonyeshwa kwenye transaction husika. Bilima inaweza kutumia providers walioidhinishwa na kuweka kumbukumbu za upatanisho.

5. Matumizi yanayokatazwa

Hairuhusiwi kufanya udanganyifu, kutuma nyaraka bandia, kujaribu kufikia data ya biashara nyingine, kuingilia usalama, kutumia jukwaa kinyume cha sheria au kuwasiliana kwa vitisho.

6. Migogoro na kusimamishwa

Watumiaji wanapaswa kuripoti tatizo kwa reference ya transaction. Bilima inaweza kuhifadhi ushahidi, kuzuia hatua hatarishi na kusimamisha akaunti wakati uchunguzi unaendelea.

7. Mabadiliko

Masharti yanaweza kusasishwa kadiri huduma, sheria au providers wanavyobadilika. Toleo na tarehe ya sasa itaonekana kwenye ukurasa huu.

Wasiliana na Bilima kuhusu sera hii